NAFASI 34 ZA KAZI SEKTA YA AFYA



Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Geita

KUMB.NA GDC/AF/MAT/V.1/6

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo ya Afya, Shirika la AGPAHI, anawatangazia wananchi wote wenye sifa ya kuomba kujaza jumla ya nafasi 34 za kazi za kada ya Afya

1. AFISA TABIBU (CO) II TGSB B TZS 680,000/= NAFASI 11

SIFA ZA KUAJIRIWA
- awe amehudhuria na kufuzu mafunzo ya utabibu (clinical medicine) ngazi ya stashahada katika chuo kinachotambulika na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU
- kutambua na kutibu wagonjwa wa kawaida
- kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake
- kufanya upasuaji mdogo
- kushiriki kupanga na kutekeleza huduma za afya ya msingi
- kueleimisha jamii na kutoa ushauri nasaha kwa wagonjwa
- kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za afya na mfuko wa jamii
- kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma
- kuanda na kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za kituo 
- kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi

2. AFISA MUUGUZI MSAIDIZI (ANO) II TGHS B TZS 680, 000/= NAFASI 11

SIFA ZA KUAJIRIWA
- Awe amehudhuria na kufuzu mafunzo ya uuguzi na ukunga (Nursing and midwifery training) NGAZI ya diploma katika chuo kinachotambulika na Serikali na kusalijiwa na baraza la wauguzi na wakunga Tanzania

KAZI NA MAJUKUMU 
- kutoa huduma za uuguzi na ukunga
- kukusanya takwimu muhimu za afya
- kuwaelekeza kazi watumishi, wauguzi walio chini yake
- kueleimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya
- kutoa huduma za kinga, tiba, afya ya uzazi na mtot
- kutoa huduma za wagonjwa majumbani na kutoa ushauri nasaha katika matatizo kwa mtu binaffsi au familia husika
- kuelekeza kusimamia mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi
- kufanya kazi nyingine atakayo pangiwa na mkuu wake wa kazi

3. MUUGUZI (NURSE) II TGHS A TZS 432,000/= NAFASI 11

SIFA ZA KUAJIRIWA
- Awe amehudhuria na kufuzu mafunzo ya uuguzi na ukunga (Nursing and midwifery training) NGAZI ya diploma katika chuo kinachotambulika na Serikali na kusalijiwa na baraza la wauguzi na wakunga Tanzania

KAZI NA MAJUKUMU
- kufanya kazi za uuguzi na ukunga na kuhudumia wateja katika ktuo ulichopangiwa
- kusimamia na kuratibu kazi za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya kazi
- kutoa huduma za wagojwa na wateja wa majmbani
- kutoa huduma za afya kinga, afya tiba, afya ya uzazi na mtoto pamoja na huduma rafiki kwa vijana
- kuelimisha agonjwa kuhusu matatizo ya kiafya
- kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi
- kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za kituo 
- kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na kiongozi wake wa kazi zinazohusiana na elimu uzoefu na ujuzi wake

MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (MAABARA) TGHS A TZS 432,000/= NAFASI 1

SIFA ZA KUAJIRIWA
- awe amefuzu mafunzo ya sayansi za maabara za afya (health laboratory sciences) ngazi ya cheti astashahada katka chuo kinachotambulika na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU
- kupima sampili zinazotolewa maabara
- kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa maabara za juu
- kuhifadhi na kufanya ukaguzi wa vitendanishi, vifaa, kemikali katika maabara
- kuweka kumbukumbu za fifaa na zana za kutolea huduma
- kufanya kazi nyingine atakazo pangiw na mkuu wake wa kazi

SIFA ZA UJUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

i/ awe raia wa Tanzania
ii/ awe na umri wa kuanzia miaka 18 na si zaidi ya miaka 45
iii/ awe na elimu ya sekondari na cheti cha taaluma cha kidato cha 6 au kidao cha 4
iv/ awe amehudhuria na kufuzu mafunzo stahili ya nafasi anayoomba
v/ awe na uwezo wa kutunza siri za wateja anaowahudumia
vi/ awe tayari kufanya kazi na kuishi mazingira yoyote hasa vijijini

ajira hizi ni za mkataba wa miezi 6 ambao unaweza kuhuishwa baada ya kipindi hiko kwisho ... waombaji watakaoitwa na kufaul zoezi la usaili watapangiwa kufanya kazi katika zahanati za NYARUGUSU, LWAMGASA, NYAMALIMBE, NKOME, KAKUBILA, NA KASOTA NA vituo vya afya vya KATORO, NZERA, KASHISHI, CHIKOBE, NA BUKOLI watumishi wanaofanya kazi kwa kujitolea watapea kipaumbele

JINSI YA KUOMBA
- andika barua ya maombi kwa mkono ukiambatanisha nakala za vyeti vyako vyote vya taaluma na ujuzi pia ambatanisha picha 2 za passport za hivi karibuni, barua zote za maombi zitumwe kwa kuwasilishwa mwenyewe mkononi ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Geita au kutumwa ka njia ya posta kwa anuani ifuatayo

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA,
"AJIRA ZA AFYA",
S.L.P 139
GEITA

AU 
tuma kwa njia ya batua pepeinfo@geitadc.go.tz

mwisho wa kupokeo maombi ni tarehe 23/03/2018 saa 9:30 AlasiriHEALTH  SECTOR EMPLOYMENT OPPORTUNITIES IN IN GEITA DISTRICT

READ MORE DETAILS AND MODE OF JOB APPLICATION

Click here to read more


Previous Post Next Post